DAKTARI WA UPASUAJI WA KINYWA NA MENO II (DENTAL SURGEON GRADE II)

Admin
Dar es Salaam
Posted on Feb 14, 2026

Job Description

1. Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa ya kinywa na meno.
2. Kutoa na kusimamia elimu ya afya ya kinywa na meno.
3. Kuboresha afya ya kinywa na meno katika eneo lake la kazi na jamii.
4. Kuziba/kukarabati meno, upasuaji, utengenezaji wa meno, kurekebisha mataya (orthodontics).
5. Kusimamia wafanyakazi walio chini yake.
6. Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
7. Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyopo eneo lake la kazi.
8. Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
9. Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
10. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya ya kinywa na meno.
11. Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya.
12. Kutoa huduma za outreach katika wilaya/mkoa wake.
13. Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
14. Kupanga na kutathimini huduma za afya ya kinywa na meno katika eneo la kazi.
15. Kufanya utafiti katika maeneo mbali mbali ya afya ya kinywa na meno.
16. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

Required Skills

N/A

Qualifications

Kuajiriwa wenye shahada ya udaktari wa upasuaji wa kinywa na meno kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali waliomaliza “Internship” na kusajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika.

Want to apply for this position?

Please sign in or create an account to apply for this job.